huduma kwa wateja

0673893283
fahamu zaid kuhusu huduma kwa wateja
Utangulizi
Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Tunduma ilianzisha kitengo cha Huduma za dharura kwa wateja (Call center) mwezi Agosti 2022 lengo likiwa kuwahudumia wateja kwa ukaribu zaidi. Kupitia kitengo hiki wateja wanapata huduma moja kwa moja ya msaada wakiwa nyumbani au popote kwa njia ya simu ya mkononi.
Kazi yake
- Kupokea taarifa mbambali kutoka kwa wateja kama za kuhusu mivujo, wizi wa maji
- Kuelemiksha wateja namna sahihi ya kufanya malipo ya maji
- Kutoa taarifa kwa wateja kama kuna hitilafu za maji / kukosekana kwa huduma katika maeneo husika
- Kushughlikia wateja ambao wanakua hawajapata ankara zao za maji kwa sababu mbalimbali.
- Kupokea Maoni / Malalamiko ya wateja na kuyawasilisha katika idara husika ili yashughulikiwa na mteja kupatiwa majibu
Muda wa kufanya kazi
Kitengo cha huduma kwa wateja kinafanya kazi kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa 4 usiku. Lengo likiwa ni kufanya kazi mpaka masaa 24 ya siku. Hivyo mteja kwa sasa atapiga simu na kupata huduma kwa muda huo.
piga simu: 0748160213/
0673893283
HABARI MPYA
mradi wa majisafi…….
habari mpya mradi wa majisafi uliokamilika mwakakati tunduma TANK LA MAJI MWAKAKATI UWANJANI Lenye uwezo wa kuchukua lita 500000 za ...
soma zaidi
soma zaidi

