Huduma za majitaka

fahamu namna huduma za majitaka zinavyotolewa

mradi wa majitaka unaoendelea

Mtandao wa Majitaka ni nini?

Mtandao wa majitaka ni mfumo au ni bomba linalopita katika sehemu mbalimbali za mitaa/ makazi ya watu kwa ajili ya kukusanya maji yaliyotumika na kuyasafirisha kwenda maeneo yaliyotengwa. Maji yaliyotumika yanaweza kuwa ni maji toka chooni, bafuni, maji yaliyooshea vyombo, maji yaliyopigia deki, yaliyofulia n.k ambayo si safi na salama.

Faida ya kujiunga na huduma ya majitaka

  • Kuzuia harufu mbaya nyumbani:-

Mara nyingi vyoo vya shimo hutoa harufu mbaya kwa sababu kinyesi hubaki palepale ndani ya shimo, pia ili nyumba yako isizungukwe na harufu mbaya ni vyema uchafu wako ukasafirishwa moja kwa moja kupitia kwenye bomba la majitaka.

  • Kinga ya maradhi/magonjwa ya mlipuko:-

Majitaka yote yatakuwa yanaondoshwa moja kwa moja kupitia bomba la majitaka, hivyo hatutegemei kuwepo kwa magonjwa kama ya kipindupindu na malaria ambayo huletwa na mazalia ya Inzi na Mbu.

  • Hakuna gharama ya kuchimba choo:-

Endapo utajiunga na mtandao wa majitaka hutakuwa na sababu ya kuchimba choo cha shimo, hivyo utakuwa umeokoa fedha nyingi za uchimbaji na ujenzi wa choo.

  • Kuepuka kutumbukia:-

Watu wengi waliojenga vyoo vya shimo ambavyo sio imara huatarisha maisha yao kwa kutumbukia endapo choo cha shimo kitatitia.

  • Paa/Bati halitaharibika:-

Nyumba nyingi zenye vyoo vya shimo mapaa (mabati) yameharibika na kutoboka kutokana na mvuke wa kinyesi cha chooni, kwa hivyo basi ili kuepukana na kufanya matengenezo ya mara kwa mara ya bati ni vyema ukajiunga na mtandao wa majitaka.

HABARI MPYA

mradi wa majisafi…….

habari mpya mradi wa majisafi uliokamilika mwakakati tunduma TANK LA MAJI MWAKAKATI UWANJANI Lenye uwezo wa kuchukua lita 500000 za ...
soma zaidi