majibu kwa maswali ya mara kwa mara
nawezaje kulipia ankara yangu?
Mteja anaweza kulipia ankara ya maji kwa mawakala wote wa Benki za Posta, NMB, NBC, na CRDB na Kupitia mitandao ya simu kwa huduma za MPESA, AIRTEL MONEY, TTCL PESA, EASY PESA, na HALOPESA. Ili kuweza kufanya malipo, ni lazima kuwa na Namba ya Malipo (Control Number) ina tarakimu kumi na mbili (Mfano: 994550451254). Kulipa kwa simu fuata hatua hizi:-
- Bonyeza: *150*00# ili kuingia kwenye menyu ya MPESA (Mitandao mingine fuata code namba husika)
- Bonyeza namba 4 (Lipa kwa Mpesa)
- Bonyeza namba 5 (Malipo ya Serikali)
- Bonyeza namba 1 (Weka namba ya Malipo)
- Ingiza namba yako ya Malipo (Mfano: 994550451254)
- Ingiza Kiasi
- Ingiza namba yako ya Siri ili kuthibitisha malipo kwenda TUNDUMA WSSA
AU:
- Bonyeza: *152*00# Kwenye simu yako
- Bonyeza namba 6 (Maji)
- Bonyeza namba 1 (Huduma za maji za pamoja)
- Bonyeza namba 3 (uliza Deni)
- Ingiza Akaunti namba yako ya maji (Mfano: J45500178012)
- Utapata deni lako
- Chagua 1 ili kulipa moja kwa moja
- Utapelekwa kwenye sehemu ya ingiza namba ya Siri ili kufanya malipo
Kwa msaada zaidi tafadhali piga simu ya ofisini kwa namba: 0748160213/
067389328
nawezaje kulipoti mivujo?
repoti mivujo kwa kupiga simu 0748160213/
0673893283
inachukua mda gani kurudi huduma ya maji mara baada ya kukatika?
Ikiwa mteja atasitishiwa huduma ya maji kwa sababu yoyote ile, huduma itarudishwa ndani ya siku 1 hadi 2 za kazi mara baada ya kulipia gharama za kurejesha huduma.
nimeletewa bili kubwa mwezi huu shida nini?
Bili inaeza kua kubwa katika mwezi Fulani kuliko miezi mingine kwa sababu zifuatazo:-
- Bomba linalodondosha maji kwa matone matone mfululizo
- Maji yanayovuja katika mtandao wa mabomba ya ndani (Internal Plumbing System).
- Kufua kwenye bomba na maji yakiwa yanaendelea kutiririka.
- Kupiga mswaki huku bomba la maji likiwa linaendelea kutoa maji. Watoto wafundishwe matumizi mazuri ya maji.
- Kutumia majisafi na salama kwa ajili ya kumwagilia bustani, maji ya umwagiliaji si rahisi kuyakadiria; inashauriwa kutumia kutumia ndoo kumwagilia (Watering can)
- Kuosha vyombo wakati maji yanaendelea kutiririka. Ni vyema kuchota maji na kuoshea pembeni.
Hivyo mteja anapaswa kuwa makini katika matumizi yake ya maji, na ikiwa bado mteja atahisi kua dira inashida, anashauriwa kupiga simu ya bure au kufika ofisini ya kanda husika.

